Familia inayoishi na chui nyumbani

Ary Borges ni jamaa kutoka Brazil anaependa wanyama kiasi cha kufikia kuishi na Chui saba nyumbani kwake.Alianza kukuza chui wawili na sasa wameongezeka na kufikia saba.

Chui hao wanaoga kwenye swimming pool pamoja nae na hata mjukuu wake humpandisha juu ya migongo yao na kuendesha kama gari!

 ''Sina wasiwasi kuhusu mabinti zangu kuwa karibu na hawa wanyama..Unatakiwa kuwaonyesha upendo na kuwaheshimu hapo ndipo utaishi nao vizuri'' amesema Ary

Yeye na mabinti zake watatu Nayara 20,Uyara 23 na Deusanira 24 huwa wanatenmbea nao na wanawapa chakula moja kwa moja mdomoni,pia wanawaruhusu kutembea ndani ya nyumba kama jikoni na hata sebuleni!

1 comment:

  1. Watongozaji wa mabinti hapa mnalo jaribu kwenda hapo lol !

    ReplyDelete