AIKA&NAHREEL: Wafungukia penzi lao na tetesi za penzi kusambaratisha PAH-ONE

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu bongo fleva ambao ni wapenzi Aika na Nahreel wamefunguka kuhusu penzi lao huku wakikana kuwa sababu ya kuvunjika kwa kundi lililokuwa linakuja kwa kasi la PAH-ONE.
Kundi hilo ambalo lilianza kushika soko la muziki huo lilivunjika huku sababu ikisemwa kuwa ni penzi la wawili hao ambalo lilitumbukiza kirusi cha chuki ndani ya kundi.

Lakini wasanii hao wapenzi wamefunguka kuwa mahusiano yao yameanza miaka sita iliyopita kabla ya kuanzishwa kwa kundi hilo kwahiyo si rahisi mapenzi yawe sababu ya kusambaratika kwa kundi hilo.
Baada ya kutokea kutoelewana ndani ya kundi wawili hao waliamua kujiweka pembeni na kuanzisha kundi lao wakiwa watu watatu 'Navy Kenzo' ambap ndani wamefanya ngoma kama 'Hold me back' iliyosemekana ni dongo kwa Pah-One japo wamekana na kusema ngoma hiyo ni maalumu kwa waliotaka kuwarudisha nyuma kimuziki.
Aika,Mie na Nahreel
Wakaenda mbali zaidi wakisema penzi lao litaishia kwenye ndoa pale mambo yatakapokamilika na wakati utakapofika wa kufanya hivyo huku wakisisitiza kuwa wanapendana kutoka moyoni.

Ngoma zao kama 'Cheza kizembe', Usinibwage na Hold me back zinafanya vizuri kwa sasa.

1 comment: