Aliyekuwa mchumba wa Balotelli aanika kisa cha kumpiga kibuti striker huyo



Aliyekuwa mchmba wa Mario Ballotelli ambaye ni mwanamitindo kutoka Ubelgiji Fanny Neguesha, amefunguka kwa nini alimpiga kibuti striker huyo mkorofi alipozungumza na Italian TV. Wapenzi hao walivishana pete ya uchumba mwaka jana mwezi March na kumwagana mwaka huohuo mwezi September.

   ‘'Hakuwa akitaka mimi nikiendelea na kazi yangu..hakupenda nifanye photo-shoots, niimbe wala nicheze. Nilijaribu kumuelewesha kuwa na mimi nna fani yangu pia lakini hakutaka kunisikiliza. Nikirudi nyuma labda niliwahisha sana vitu ..pengine ningesubiri kidogo kabla ya kukubali ombi lake la uchumba. Alikuwa na kichwa kigumu hakutaka kabisa kuelewa kuwa mimi pia nna fani yangu na inatakiwaiendelee pia. Mwisho wasiku nilimrudishia pete ya uchumba aliyonivisha, ali-mind lakini kwa sasa kila mtu anafanya yake'' Alifunguka Fanny.

0 Maoni:

Toa Maoni