Baada ya Jay Z kula kipondo kutoka kwa shemeji yabainika ndoa yake na Beyonce si shwari hata tattoo zinazofanana hazipo tena!

Saa nyingine picha huwa zinaongea mengi sana kwa kuzitazama tu, na kama ni hivyo basi couple yenye nguvu zaidi  Jay Z na Beyonce mambo yao ya ndoa si shwari baada ya picha kuonyesha tattoo zinazofanana zenye alama 'IV' walizokuwa nazo kwenye vidole vyao vya mkono wa kushoto kile kinachovaliwa pete ya ndoa hazipo tena! 



Alama hiyo ya kirumi IV maana yake ni namba 4 na namba nne kwao inaendana na matukio muhimu September 4 ni siku ya kuzaliwa kwa Beyonce, December 4 ni birthday ya Jay Z huku ndoa yao ilifungwa April 4.

Na kutoweka kwa tattoo hizo kumegundulika mwezi mmoja uliopita.


0 Maoni:

Toa Maoni