Lulu aonyesha Tatoo nyingine yenye ujumbe kwa masnitch!

Msanii mdogo lakini anayefanya vizuri katika kiwanda cha filamu Tanzania Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu jana kupitia mtandao wa Instagram ame-share picha na mashabiki inayoonyesha tattoo yake nyingine iliyochorwa juu kidogo ya kifua iliyoandikwa 'only God can judge me'.

Lulu hakutuma picha tupu,chini aliandika ujumbe mreefu! Cheki picha na alichokiandika kwenye picha hiyo.

hotlulumichael
Kumekuwa na kawaida ya watu kuongea na kuhukumu wenzao bila ya kujua wanachokiongelea pengine!!Kwa upeo Wangu mdogo nafahamu sisi wote ni binadamu na tunamtegemea mtu mmoja MWENYEZI MUNGU...lakini cha kushangaza Kuwa watu wako busy kuhukumu wenzao kuliko hata huyo mwenye cheo chake...Hivi Mungu angetaka kufanya Kama wanadamu tunavyofanya kungeangaliana kweli....Nadhani umefika wakati wa kumuachia mwenye majukumu yake kufanya kazi...tuache kujipa u busy usio wa lazma....!!!ONLY GOD CAN JUDGE ME....Gud nyt fam👋

0 Maoni:

Toa Maoni