Ngono kuonyeshwa hadharani katika kipindi cha mapenzi!

Kipindi kipya cha TV kimeleta utata mkubwa huko Uingereza.

Kipindi hicho kimepewa jina la Sex Box,ni kipindi kipya cha mapenzi kinachohusisha couple tatu ndani ya box hilo lililotengenezwa kama nyumba ambalo lipo kwenye stage mbele ya studio ambayo pia kunakuwepo na audience,huku kukiwa na jopo la wataalamu.

Nyumba hiyo"sex box" imetengenezwa kwa mbao laini na kwa ndani inaonekana kama chumba cha hotel, pia imetengenezwa kwa soundproof kwahiyo wapendanao wanaoingizwa humo hawasikii chochote wala kuona lolote linaloendelea nje.

Wakati wapenzi hao wapo ndani ya box ambapo wanapewa muda wa dakika 30, Mariella Frostup ambaye ndiye muongozaji wa show hiyokwa kushirikiana na wataalamu Dan Savage na Phillip Hodson wanajadiliana mambo kuhusiana na wapenzi hao waliomo ndani.

Kwa mfano kama moja ya couple ni ya vijana wadogo inaweza kuwekwa mada ikachangiwa kuhusu namna ngono na madhara yake kwa kizazi hicho na nini kinaweza kufanyika ili kufanya matamanio ya ngono kwa wasichana kuchukua muda mrefu na mada hiyo inajadiliwa na watu wazima waliopevuka.

Lakini pia inawezekana kujadiliana hata kuhusu kitu gani wanakipata kitandani wapenzi wa jinsia moja wanaume yaani ushoga.

Ni majadiliano ambayo yanakuwa hot na yenye kuvutia lakini pia yanayoelimisha,kuleta changamoto na hata zile couples zinapotoka kwenye sex box unasahau kama walikuwemo ndani.

Lakini mwisho Camera inakwenda ndani ya sex box na watazamaji wataamua nani amefanya vizuri zaidi,nia ni kufanya kuwa kionekane ni kitu cha kawaida na halisia kuliko kwenye mikanda ya ngono.

0 Maoni:

Toa Maoni