Dah sasa huku ni wapi...Binti wa R Kelly ajigeuza dume!

R Kelly na Jaya kipindi bado mdogo
Nikivuta picha miaka mitano ijayo kizazi chetu kitakuwa wapi sipati picha! Binti wa mwisho wa staa wa muziki wa RnB wa kitambo R.Kelly anayeitwa Jaya Kelly ameonekana kuwa hajaridhishwa na jinsia yake hivyo akaamua bora awe kidume!
Jaya ambaye anamiaka 14 kwa sasa anajivunia muonekano wake na lifestyle anayoishi kama mvulana huku akijipachika chata ya FTM yaani 'Female To Male Transgender' huku sasa akijiita Jay badala ya Jaya!

Ndoa ya zamani ya R.Kelly na Andrea  Kelly ndio ilizaa matunda haya ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu Robert Kelly Jr., Joann Kelly na Jaya Kelly. Cheki picha za Jaya akiwa katika muonekano wa sasa ambao anaufurahia zaidi wa kiume.

Jaya,dada na mama yao
Hapa ni watoto wa R.kelly na mama yao kabla mambo hayajaharibika

0 Maoni:

Toa Maoni