Picha hii iliyopigwa usiku wa tuzo za Oscar na yavunja record na kusababisha huduma kusuasua kwa muda!


Wakati wa tuzo za Oscar zilizofanyika jana usiku mmiliki na muendeshaji wa kipindi cha The Ellen Degeneres show  Ellen mwenyewe alipiga picha maarufu kama Selfie akiwa na mastaa kibao Brad Pitt, Angelina,Jenniffer Lawrence, Julia Roberts,Lupita Nyongo'o na wengine na kui-share katika mtandao wa twiter na kuifanya picha hiyo kuvunja rekodi yakuwa maarufu mtandaoni baada ya kuwa re-tweeted mara nyingi sana.. 
Tweet hiyo yenye picha ya Selfie ilipata watu zaidi ya milioni mbili walioi-retweet na kuvunja rekodi iliyoshikiliwa na picha iliyowahi kutumwa na raisi wa Marekani Obama... Pia ilisababisha huduma ya twitter kusuasua kwa muda!!

0 Maoni:

Toa Maoni