TANZIA: Hii imenitoa chozi!


Mimi mwenzenu ni mpenzi sana wa tamthilia tena wakati mwingine huwa nafatilia zile za Telemundo na Televisa na moja kati ya tamthilia nilizowahi kuangalia nikaipenda ni El cuerpo del deseo (Second chance) ambayo ilichezwa na Mario Cimmaro alikuwa anatumia jina la Salvador kwenye hii second chance, Lorena Rojas alikuwa anatumia jina la Issabela na wengine kibao.

Sasa katika pitapita zangu kwenye mitandao si ndio nikakutana na habari hii ya kusikitisha kuwa Isabela (Lorena Rojas) amefariki dunia! Lorena alikuwa ni mgonjwa wa kansa tangu mwaka 2008 na ilianza kama kansa ya matiti lakini ilisambaa katika sehemu nyingine za mwili na kushambulia mpaka maini. Kwa hiyo kuanzia hapo alikuwa akiendelea na matibabu na afya yake ilikuwa safi tu mpaka safari yake ilipofika mwisho mwaka  huu tarehe 16 february siku ya jumatatu...sad!

Lorena ambaye ni raia wa Mexico alikuwa ni mwigizaji na mwanamuziki pia na hata katika soundtrack ya Second chance aliimba yeye pale kwenye sauti ya kike. Nimesikitika sana maana nampendaje sasa huyu dada ila kazi ya Mungu haina makosa na duniani sisi ni wapitaji tu. Ina lillah waina Illah Rajiun.. Mungu amlaze mahala pema!

Hii ni ndio ile Second chance sasa.


0 Maoni:

Toa Maoni