Mafanikio yanazidi kunyooka kwa wasanii Nigeria

Tukizungumzia muziki barani Afrika moja kati ya nchi zinazofanya vizuri na mziki wake unavuka boda huwezi kuacha kuizungumzia Nigeria. Ukimuacha wanamuziki kama 2 Face,P sguare ambao walifungua njia sasa kuna kizazi kipya kinachofanya vizuri sana Wizkid, Davido ,Iyanya,Tiwa savage, Banky W , K Cee na wengine kibao na wana mafanikio ya kutosha!

Jana kupitia istagram mwanadada Tiwa savage first lady wa Marvin records ya Don Jazzy ameshare picha akisaini deal la mahela mengi baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa MTN.Kupitia vyanzo vya kuaminika deal hilo ni la kama naira milioni 30 hivi!


Hivi karibuni pia mwanamuziki Iyanya alisign deal la kuwa balozi wa MTN pia kwa dau kama la naira milion 60 hivi..Cheki picha

Wengine waliosign deal hilo ni Davido na Kcee..Mfano mzuri na wa kuigwa kwa makumpuni na wasanii hapa Tanzania.

0 Maoni:

Toa Maoni