Tukio hilo ambalo mbali na kuthibitishwa na mtoto mwenyewe, pia limeelezewa na majirani wa mzee huyo ambao kwa majibu wa maelezo yao wanadai kwamba kitendo hicho kimesababisha mtoto huyo kutoroka kwao na kwenda kuishi mitaani.
![]() |
| Mtoto anayedaiwa kulawitiwa na baba yake |
"Kutokana na hali hiyo mtoto huyu amekuwa akilala mitaani na mara nyingi huwa analala nyuma ya nyumba yangu huku akijifunika magunia," alisema mama mmoja wa Kimara Msewe huku akimuonyesha mwandishi wetu eneo hilo.
![]() |
| Mtangazaji wa Times Fm, Edson Mkisi Jr akiwahoji mashuhuda wa tukio hilo |
Akizunguamza na mtangazaji wa Radio Times kupitia Kipindi cha Hatua Tatu, Edson Mkisi Jr, mtoto huyo alisema amekuwa akingiliwa na baba yake huyo mara kwa mara na kumsababishia maumivu makali kiasi cha kusababisha kushindwa kwenda shule."Nilikuwa nasoma darasa la pili Msewe lakini niliacha shule baada ya baba kuanza kuniingilia nyuma mara kwa mara," alisema mtoto huyo.
Nae mjumbe wa serikali za mitaa mtaa wa Msewe, Saimon Kachwele, alisema tukio la mtoto huyo si geni ofisini kwake na ni kama limekuwa sugu kutokana na kila wakati kushughuklikiwa sehemu mbalimbali hadi vituo vya polisi lakini kushindikana. Alipoulizwa kuhusu madai ya kwamba baba yake ndio amekuwa na tabia ya kumuingilia kinyume na maumbile, Kachwele alise ahilo halijui ila anachojua ni kwamba tukio la mtoto huyo kukimbia kulala nyumbani kwao ni la kawaida na hata baba yake analijua.
"Kusema kwamba baba yake ndio anayemuingilia kusema ukweli hilo sijui ila ninachojua ni kwamba mtoto huyo kutolala kwao ni tukio la kawaida na sisi kama serikali tumeshaangaika nalo sana lakini tumeshindwa kabisa," alisema mjumbe huyo.
![]() |
| Mjumbe wa eneo hilo (mwenye nguo nyekundu) alithbitisha tukio hilo |
![]() |
| Mashuhuda |





Kwakweli huyo Baba inabidi achukuliwe hatua kali Sana hawezi mfanyia mwanawe wa kumzaa mwenyewe kitendo Hicho
ReplyDelete