Tamaa ya kujibadili jinsia yamponza..atamani kufa!

Raia wa Belgium Nathan Verhelst mwenye umri wa miaka 44 amechagua kifo baada ya oparesheni kamili ya kubadili jinsia aliyofanyiwa kutoka mwanamke kuwa mwanaume kumfanya awe kioja!


Alizaliwa na jinsia ya kike na akapewa jina la Nancy na alitamani kuwa msichana baada ya kuona kaka zake kama wanapata upendeleo katika familia.

Process za kubadilishwa kwake jinsia kulianza kwa kupewa hormone therapy mwaka 2009,ikafatiwa na operation ya mwisho ambayo haikuwa na matokeo mazuri iliyofanyika mwaka uliopita ya kutengeneza sehemu za siri.

 Muda mchache kabla ya kifo chake Nathan alisema
 "Nilikuwa msichana ambaye hakuna anyenitaka wakati kaka zangu walikuwa wanasherekea..mama yangu alikuwa analalamika kila mara 'Laiti ungekuwa mwanaume' ....nilikuwa tayari kusherekea kuzaliwa upya kama mwanaume lakini nikijiangalia kwenye kioo najiona kituko..maziwa yangu sio mazuri kama nilivyotaka..utupu wangu mpya una kila dalili ya kunikataa..sitaki kuwa kioja!" Alisema Nathan.

Baada ya kutoridhishwa na muonekano wake baada ya kujibadili Nathan akaomba madaktari wamchome sindano ya sumu afe!

0 Maoni:

Toa Maoni