Nyerere amesema filamu za bongo haziingizi kipato kikubwa kiasi cha kufanya mambo makubwa wanayoyataka au kumiliki mali kiasi kikubwa na ndio maana ili waendane na maisha ya kuigiza wanalazimika kukubali kutumika na wanaume mbalimbali ili kuingiza kipato na kuishi katika maisha hayo.
"Unajua hizi filamu zina namna yake na sio kwamba zinalipa kihivyo kusema hawa dada zetu waishi maisha hayo tunayoyaona kwa baadhi yao,lakini inabidi tu wakubali kutoka na wanaume wenye uwezo wa kuwapa hicho kidogo wanachotamba nacho wakiachwa wanalazimika kutafuta mwingine,hii ni kwasababu kutengeneza movie ni gharama kubwa inahitaji mtaji mkubwa ili upate faida nzuri"alisema Nyerere.
Anaongeza kuwa wengi wa wanawake waliopo kwenye bongo movie au wanaokimbilia kwenye bongo movie wanataka kuuza sura tu na si watendaji kazi wa kweli na ndio maana kwasasa pia kuna utitiri wa wanawake ambao wanaibuka kusikojulikana nao wanapewa nafasi ya kucheza movie.
Kumekuwa na maneno mengi kwasasa kuhusu tabia za wanawake wengi wa bongo movie kufanya vitendo visivyofaa kwenye jamii,wengine wakidaiwa kufanya hata biashara ya kujiuza kiaina ili kujiingizia kipato na kuishi maisha ya ufahari kitu kinachoichafua bongo movie.
0 Maoni:
Toa Maoni