Diamond ni habari nyingine sasa...cheki video gumzo Africa ya wasanii 19 akiwemo!


Akiwa nchini Nigeria sasa kwenye muendelezo wa shughuli zake za muziki, Diamond Platnumz anazidi kula shavu kwa kufanya kazi na wanamuziki na ma-prodyuza maarufu na wakubwa Nigeria na Afrika kwa ujumla.

Kupitia Instagram jana prodyuza mkubwa na mwanamuziki pia kutoka Nigeria Don Jazzy ali-share picha inayomuonyesha akiwa studio na Diamond na ikumbukwe Don Jazzy ameshafanya kazi na wasanii wakubwa ikiwemo D'Banj aliyefanya nae hit songs kama Fall in love,Oliver Twist n.k.


Pia Diamond Platnumz ni miongoni mwa wanamuziki 19 wa Afrika waliochaguliwa kukutana nchini Nigeria ili kushiriki katika wimbo wa pamoja wa kuhamasisha vijana kujiunga na kilimo cha kakao na chocolate,katika kampeni ya Do Agric yaani Do Agriculture na hivi karibuni Diamond alikuwa nchini Afrika kufanya shooting ya wimbo wa Cocoa and Chocolate akiwa na AY pia.

Wasanii walioshiriki ni D’Banj (Nigeria), Buffalo Souljah (Zimbabwe), Judith Sephuma (Afrika Kusini), Vusi Nova (Afrika Kusini), Liz Ogumbo (Kenya), Nancy G (Swaziland) , Dama Do Bing (Msumbiji) , Diamond (Tanzania), Femi Kuti,(Nigeria) Rachid Taha (Algeria), Juliani (Kenya), Omawumi (Nigeria), Tiken Jah Fakolyu (Ivory Coast), Fally Ipupa (DRC), Kunle Ayo (Nigeria), Omawumi (Nigeria) AY (Tanzania), Wax Dey (Cameroon), Victoria Kimani (Kenya) na Dontom (Nigeria).

Icheki video hii na u-enjoy ijumaa ya leo.

           

0 Maoni:

Toa Maoni