Mpenzi wa Ronaldo ashambuliwa baada ya kushiriki kampeni ya wasichana waliotekwa akiwa mtupu!

Wakati bado wakiwa kwenye majonzi ya kupoteza zaidi ya wasichana 200 walioshikiliwa na kundi la Boko Haramu huko nchini Nigeria, Mwanamitindo mwenye asili ya Russia Irina Shayk ambae ni mpenzi wa mwanasoka maarufu Christiano Ronaldo ame-share picha inayomuonyesha akiwa mtupu huku kajiziba na bango linalosapoti kampeni ya kurudishwa kwa mabinti hao #BringBackOurGirls kitu kilichokera watu.

Baada ya picha hiyo binti huyo wa miaka 28 alicharukiwa na mashabiki waliomkashifu kwa kutoonyesha kuwa anamaanisha alichoandika kwenye bango hilo na haya ni baadhi ya makavu aliyopewa.

"Pretty tasteless and disrespectful. No class. This is exactly the justification terrorists are probably using to prevent women from receiving 'western education,'
 

''Would you stand there naked wishing sorrow on the 9/11 victims? Would you do it for the tsunami? This is a tasteless attitude to 200 missing girls''


Wanafunzi zaidi ya miambili walitekwa nyara wiki jana na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram na kuwapeleka msituni.Baadhi ya wasichana hao walifanikiwa kutoroka lakini wengine wengi wangali wanazuiliwa.

Wapiganaji hao wamesababisha vifo vya maelfu ya watu nchini humo wakidai kuwa wanapigania kile wanachosema ni misingi ya dini ya kiisilamu.
Mastaa kibao kote duniani wameungana kwa pamoja katika kampeni ya kurudishwa kwa wasichana hao.

Tonto Dikeh
Puffy Daddy
Michelle Obama

0 Maoni:

Toa Maoni