TANZIA: Unamkumbuka Amina Ngaluma aliyeimba Mgumba No.1? Hatunaye tena duniani..

 Mmoja wa waimbaji nyota wa muziki wa dansi waliowahi kutokea hapa nchini Amina Ngaluma a.k.a JAPANIZ amefariki dunia.

Muimbaji huyo alitamba na bendi za Tam Tam na Double M Sound,amefia nchini Thailand alipokuwa akiishi kikazi kwa muda mrefu.Moja ya nyimbo zilizompa umaarufu ni Mgumba No.1 aliouimba na bendi ya African Revolution 'Tam Tam' chini ya Mwinjuma Muumin.

Amina Ngaluma aliyesimama

Tungependa kuwapa pole ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa familia,mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.
Habari kwa hisani tovuti ya Times fm.

0 Maoni:

Toa Maoni