Khloe na French Montana waingia midomoni baada ya kutupia 'mguu wa kuku' kwenye mtandao

 
Khloe Kardashian na mpenzi wake wa sasa rapa French Montana wameingia midomoni mwa watu baada ya kutupia picha kwenye mtandao inayoonyesha French akiwa kashika 'mguu wa kuku' (bunduki) huku Khloe akiwa na kinywaji kwenye chupa ya Champagne.

Inasemekana walikuwa kwenye maandalizi ya video ya French "They Don't Love You No More " huko Miami, Florida siku ya jumapili.

Mashabiki wa Khloe wanasema Montana ameshaanza kuwa mfano mbaya kwake kwa kuwa Khloe sio wa mambo hayo na maisha yake yote ya ustaa hajawahi kutengeneza headlines kwa skendo mbaya kama dada yake Kim.

Hizi ndio picha zilizozua gumzo

0 Maoni:

Toa Maoni