Nando: Nimeacha kutumia 'Unga' lakini bangi..halafu namzimia Lulu ile mbaya!

Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa za kulevya.

Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha 100.5 Times Fm, Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa kuacha.
Mimi na Nando studio leo
Edson Mkisi Jr
Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.

“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pee pressure na watu niokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi...ni yale maisha ya kujiachia.” Amesema Nando.

Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana na dawa za kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza idadi.

“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au mbili kwa siku.”

Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye kibali cha kuvuta bangi katika jimbo la California kwa maelezo ya daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.

Kuhusu uhusiano na Dayna amefunguka kuwa wako kikazi zaidi na ni majirani kwa hiyo hamna cha zaidi huku akianika kweupe kuwa anamzimia staa wa Bongo movie mwenye mvuto Elizabeth Michael a.k.a Lulu kwa sababu ni mchapakazi na  ana mvuto na  yuko tayari kutulia na kutangaza ndoa kama Lulu atakubali ombi lake!

0 Maoni:

Toa Maoni