Serikali haiutambui uchawi!! Kama unaamini hivyo inabidi umuone mwanasheria akueleze vizuri, linapokuja suala la kukutwa katika mazingira ya kichawi au ukisababisha madhara ya uchawi huo, utaeielewa sentensi hiyo ndivyo sivyo.
Mtanzania mmoja alijulikana kwa jina la Amos Chipeta aliyekutwa na hatia ya kujihusisha na uchawi na kumlaghai mwanamke mfanyabiasha raia wa Kenya na kumuibia shillingi milioni tisa.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, mchawi huyo alimlaghai mama mmoja wa Kenya aliyefahamika kwa jina la Catherine Njeri kuwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu, yaani milioni 18.
Baada ya kukamatwa February mwaka huu, Chipeta na mwenzake Peter Christopher walikutwa na hirizi zinazosadikika kuwa hutumika kufanyia uchawi pamoja na vifaa vingine.
Kwa pamoja walijitetea kuwa mwanamke huyo ndiye aliyewafuata na kuwaomba wazifanye fedha hizo kuwa maradufu, lakini mahakama ikawakuta na hatia na kutupilia mbali utetezi wao.

CREDIT KWA TOVUTI YA TIMES FM TZ

0 Maoni:
Toa Maoni