Picha yamponza Beyonce achanwa kuwa anaji-edit..


Jana mashabiki walimshambulia Beyonce kwa picha aliyopost kwenye Tumblr ikiwa ni moja kati ya picha za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alizopiga mapema mwezi huu, ikimuonesha akishuka ngazi akiwa ndani ya vazi la ufukweni. (Icheki chini hapo)


Madai ya mashabiki hao yaliyowekwa kwenye mtandao wa TMZ pamoja na picha ni kwamba Beyonce ali-edit sehemu iliyoonesha nafasi kati ya mapaja yake ili aonekane mwembamba zaidi..

Hizi ni baadhi ya comment za kumchana baada Bey baada ya kutupia picha hiyo..

-*Why the hell is Beyonce photoshopping in a thigh gap?’  
-*Questionable thigh gap there, Bey. #photoshop #wonkystep #beyonce’.
-*beyonce needs to chill out forever photoshopping a thigh gap’
-*@Beyonce uses photoshop!! Why promote accepting yourself in your videos if you clearly lie about yourself?’


Masaa machache baada ya tuhuma hizo kuenea, Beyonce aliamua kujibu kwa vitendo kwa picha zinazoonesha uhalisia wa mwili wake na kwamba hakuna ‘Photoshop’..


Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki kumtuhumu Beyonce na Jay Z kufanya photoshop ya picha zao ili aonekane mwenye mvuto zaidi.

0 Maoni:

Toa Maoni