Nahodha Wa Bafana Bafana Auawa Kwa Kupigwa risasi akimtetea mpenzi wake


Mlinda mlango wa klabu ya Orlando Pirates ya Afrika kusini Senzo Robert Meyiwa, amefikwa na umauti baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwishoni mwa juma lililopita wakati akimlinda mpenzi wake Kheli Khumalo asijeruhiwe na  watu hao waliokuwa wamemshikia silaha na kutaka kufanya uhalifu. 

Mda mfupi kabla ya kufikwa na umauti mpenzi wake alipost picha hii wakionekana wenye furaha
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jeshi la piolisi nchini Afrika kusini Meyiwa alifikwa na mkasa wa kupigwa risasi baada ya watu wawili kumvamia katika nyumba aliyokuwa amepumzika maeneo ya Valorous, nje kidogo ya jiji la Johannesburg.

Taarifa ya jeshi la Posili imeendelea kubainisha kwamba tukio hilo lilijitokeza mishael ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika kusini ambapo imethibitika watu hao wawili walioingia ndani waliongozana na mtu mwingine ambae alibaki nje ya nyumba iliyoshuhudia tukio hilo ambapo waliingia na kutaka kupewa simu za mkononi,pesa na vitu vingine vya thamani.

Hata hivyo Meyiwa aliaga dunia baada ya kufikishwa hospitalini.

Jeshi la polisi nchini Afrika kusini limeahidi kufanya jitihada za kuwasaka wahalifu waliohusika na tukio la kifo cha mlinda mlango huyo alieaga dunia akiwa na umri wa miaka 27.

Siku ya jumamosi Meyiwa alikuwa sehemu ya kikosi cha Orlando Pirates wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi huko Afrika kusini. 
Mpenzi wake wakati mjamzito
Hapa akiwa na mtoto wake

0 Maoni:

Toa Maoni