FIFA YASEMA KOMBE LA DUNIA 2014 KAMA KAWAIDA BRAZIL

Katibu mkuu wa Shirikisho la sika la dunia Fifa ,Jerome Valcke amesema kombe la dunia 2014 zitafanyika nchini Brazil kama kawaida japo amekiri kuwa amekuwa na mazungumzo na serikali ya nchi hiyo kuhusu kusitisha mashindano yanaoendelea ya Confederations Cup kwasababu ya mgomo wa wananchi wa nchi hiyo.

Valcke anasema usalama wa kombe la dunia2014 ni mkubwa na tayari serikali imethibitisha kuhusu hilo.

Kumekuwa na mgomo na maandamano katika miji ipatayo 100 nchini Brazil wakipinga gharama kubwa za maisha ikiwemo kupanda kwa nauli kwasababu ya fedha nyingi iliyotumika kwenye ukarabati wa viwanja vitakavyotumika kwa kombe la dunia 2014.

0 Maoni:

Toa Maoni