HALI YA MANDELA BADO TATA

Rais mstaafu wa Africa Kusini Nelson Mandela, bado anaelezewa kuwepo kwenye hali mahututi ingawa madaktari wanaendelea kumuangalia kwa karibu.
Mpaka kufikia usiku wa kuamkia leo taarifa kutoka kwa Rais wa Africa Kusini Jacob Zuma imesema kuwa madaktari mjini Pretoria wanaendelea na juhudi za kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida.
Mandela anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa huko Mediclinic Heart Hospital iliyopo nchini Africa Kusini.






















0 Maoni:

Toa Maoni