Aibu: Mshiriki kutoka Tanzania Nando atimuliwa katika jumba la Big Brother

Baada ya kukaa katika jumba la Big brother kwa muda mrefu na zikiwa zimesalia wiki chache kufikia fainali,Mtanzania Ammy Nando au Nando jana ametolewa katika jumba hilo baada ya kukiuka taratibu na masharti yaliyowekwa ambapo ukivunja unapewa onyo ambalo likifika mara tatu unatolewa.

Baada ya kupewa onyo la kwanza alipohudhuria party ambazo hufanyika kila jumamosi akiwa na silaha yaani kisu (kitu ambapo hakiruhusiwi) wiki chache zilizopita,Nando alipewa onyo la pili baada ya kugombana na Elikem ambaye ni mshiriki kutoka Ghana na kumtolewa maneno mazito ya kumtishia  maisha “I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die.” .

Na jana Nando akapewa onyo la mwisho baada ya kukutwa analala na mkasi chini ya kitanda chake onyo lililoambatana na kuwa disqualified katika jumba la Big Brother. Nando hakuruhusiwa kuaga washiriki wenzake ambapo Head Of House Bimp ambae ni mshikaji mkubwa wa Nando akapewa amri na Big Brother ya kukusanya mizigo yote ya Nando na kuiwasilisha Diary room.

Hii ni mara ya pili kwa mshiriki kutoka Tanzania kuwa disqualified baada ya mwaka juzi Lotus aliyeiwakilisha Tanzania kugombana na mshiriki kutoka kutoka Africa Kusini Luclay na kutimuliwa kama ilivyokuwa kwa Nando.

0 Maoni:

Toa Maoni