Kutoka BBA: Annabel wa Kenya na Sulu waaga shindano

Mshiriki kutoka Kenya aliyekuwa kasalia katika jumba la Big brother Anabel Mbaru naye kaaga shindano la Big Brother the Chase akiwa na mshiriki kutoka Zambia Sullu.Hiyo inafanya Kenya kuaga rasmi shindano na Zambia kubaki na mshiriki mmoja ambaye ni Cleo.

Anabel

Sulu

Kila jumapili eviction hufanyika ambapo washiriki wawili wanaokuwa Nomonated huaga shindano.Kitendo cha Sulu kutoka ambae alikuwa maarufiu kwa uchekeshaji kimefanya washiriki kupata hofu kwa kuona shindano halitabiriki kwa sasa baada ya wiki iliyopita Bassey kutoka Siera Lione ambaye pia alikuwa ni mmoja ya waburudishaji nae  kuaga.

Tanzania imebakiza na mshiriki mmoja tu anayewakilisha ambaye ni Feza baada ya Nando kuwa disqualified kwa kuvunja masharti.

0 Maoni:

Toa Maoni