Baada ya Snura na Shilole sasa ni zamu ya Mzee Magali!

Sasa imekuwa ni kawaida kusikia wasanii wa filamu kuingia kwenye muziki.Tulianza kwa kumsikia Shilole wakaja Nisha na Flora Mvungi  baadae Snura na sasa ni zamu ya mkongwe wa maigizo nchini  Charles Magali maarufu kama mzee Magali!

Mzee Magali katika studio za Times fm
Unaweza kushangaa baada ya kusikia habari ya mzee Magali kuimba ila ndio habari hiyo na tayari ana wimbo wake mpya ambao kautambulisha leo kupitia Times fm unaitwa DAR RAHA. Akiongea kwenye kipindi cha Hatua Tatu cha Times fm,amesema video ya wimbo huo inakuja pamoja na album yenye nyimbo sita baada ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  yaani mwezi wa nane.

Mzee Magali naDj R guy, Mkisi na mie
Anasema ana kipaji cha kuimba toka alipokuwa mdogo ila aliamua kuingia katika uigizaji kwa ajili ya maslahi.Amefunguka kuhusiana na lafudhi yake pia na kusema sio Mkongo kama watu wanavyodhani ila tu anaitumia katika kuigiza. Asili yake ni mluguru kutoka Morogoro.Aliamua kutumia lafudhi hiyo baada ya kukutana na mzee wa kikongo hotelini akizungumza na msanii Ray Kigosi kumshauri aitumie maana itamtoa.

Anasema yeye ndio Koffi Olomide wa Bongo watu wakae tayari kwa ujio wake na baada ya mwezi mtukufu atadodosha shoo ya kufa mtu.

2 comments:

  1. pigeni kazi nawakubali sana times yaani hata kama nikiwa nimekasirika nikisikiliza hatua tatu tu najisikia mwenye furaha ya jabu nawapenda sana jamani.

    ReplyDelete