Hongera kwa vichuna wa Times fm kwa kuaga ukapera

Weekend ilikuwa nzuri kwa baadhi ya watangazaji wa Times fm  baada ya kuaga ukapera .Ijumaa mtangazaji wa kipindi cha sunrise Samira Suleimani alifunga ndoa huko visiwani Zanzibar.

Samira na mume wake
Pia msanii mkongwe wa filamu na mtangazaji wa kipindi cha Filamonata Susan Lewis maarufu kama Natasha nae alifunga ndoa katika kanisa la mt. Joseph hapa mjini Dar es salaam.

Natasha na mumewe na mtoto wake Monalisa

Ndoa ni jambo la kheri, Mamu Africa inawatakia kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa na mdumu inshallah.

0 Maoni:

Toa Maoni