![]() |
| Bella katika studio za Times |
![]() |
| Baada ya kipindi tukapata picha |
![]() |
| Mie na Bella |
Akizungumzia kuhusu muziki,Bella anasema ameamua kuingia rasmi kwenye muziki na kashatoa single yake kama solo artist inayoitwa 'Jikubali mwenyewe' ambayo inapatikana kwenye audio na video.Kutoa singo kama solo artist haimaanishi kuwa katoka kwenye kundi lao la muziki Scorpion Girls ila tu ni katika kukuza muziki wake zaidi huku Kalama akiwa ni meneja wake.Anasema yeye na Luteni kalama wana mipango mingi ikiwa kufunga ndoa na kutengeneza familia.
Pia akizungumzia Scorpion girls,anasema kundi hilo lipo na linaundwa na wasanii wengi tu akiwemo yeye mwenyewe,Kabula,Jacky Pentizel,Aunt Lulu, Sajenti na wengine.
Akizungumzia maneno yaliyozagaa kuhusu kugombana na Kabula na kumtupia vitu nje,Bella anasema ni kweli waligombana sababu ikiwa ni Kabula kumtukana matusi mazito baada ya Bella kumsifia mwana Scorpion mwenzao Jacky Pentizel kwa kununua gari.Ila anasema hajawahi kumfukuza wala kumtupia vitu nje Kabula maana hawaishi pamoja yeye anakaa na familia yake.





MAMU KITOSI UMEPENDEZA MASHAALLAH NATAMANI RAMADHANI ISIISHE ILI UWENDELEE KUVAA HIVI.
ReplyDelete