Amuua mkewe kwa kipigo kisa nyoka wa kimila

Mwanaume mmoja nchini Nigeria Godwin Idon anashikiliwa na Polisi baada ya kumpiga mke wake na kumuua kwenye kijiji cha Edo baada ya mtoto wake wa kiume kumuua nyoka kwenye chumba wanachoishi.

Ugomvi mkubwa ulitokea baina ya wawili hao muda mchache baada ya mtoto huyo kumuua nyoka chumbani.

Mwanaume huyo inaelezwa kuwa amefanya hivyo kwasababu za kimila.

Wiki moja tokea wawili hao waligombana,mke wake akiongozana na mama mkwe wake waliamua kutafuta ushauri kwa waganga wa kienyeji kujua kwanini mwanaume huyo aliamua kumpiga mke wake kwasababu ya mtoto kuua nyoka chumbani.

Mke aliporudi nyumbani ndipo akakutana na kipigo cha mume wake aliyemgonga kichwani na kuzimia kabla ya baadaye kupoteza maisha.

Mwanaume huyo sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi.
 


0 Maoni:

Toa Maoni