Nando atua Bongo kimya kimya

Aliyekuwa mshiriki wa Tanzania kwenye mashindano ya Big Brother Africa ambalo safari hii linajulikana kama Big Brother the Chase Nando aliyetimuliwa katika jumba Jumatatu wiki hii amerejea nyumbani Tanzania kimya kimya.

Nando alipokelewa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na afisa uhusiano wa Multchoice Tanzania Barbara Kambogi.

Barbara amethibitisha kumpokea Nando kutokea nchini Africa Kusini,akifafanua kuwa amepokelewa kimya kimya kwasababu ametoka kwenye jumba hilo la Big brother kwa kutimuliwa kitendo ambacho hakipaswi kuungwa mkono.

Amesema Nando pia hatafanyiwa sherehe zozote kwasababu ya namna alivyotoka kwenye jumba hilo,vitendo ambavyo vilikuwa kinyume na taratibu za shindano hilo.

Nando alitolewa kwenye jumba hilo kwa kuvunja masharti ya shindano ikiwemo kutimiza makosa matatu ambayo hutakiwi kuyafanya,ikiwemo ugomvi wake na Elkeem kiasi cha kutishia kuua akisema watu kama hao wanastahili kufa na pia aliwahi kuingia disco akiwa na kisu.
Nando si mshiriki wa kwanza kutimuliwa kwenye jumba la Big Brother,itakumbukwa mwanadada Lotus naye alitimuliwa kwa kumchapa mshiriki mwenzake makofi.

Mshindi wa mwaka huu atajikusanyia kitita cha dola 300,000 zaidi ya shilingi milioni 450 za Tanzania.

0 Maoni:

Toa Maoni