Kutoka BBA:Hatimaye Pokello aaga shindano

Baada ya kuwa nominated mara nyingi katika jumba la Big brother hatimaye mwanadada mrembo raia wa Zimbambwe jana ameaga rasmi shindano hilo jana.Bassey kutoka Siera Lione naye aliungana na Pokelo na kufanya Zimbambwe na Siera Lione kuaga rasmi shindano hilo.



Kama utakumbuka Hakeem kutoka Zimbamwe na Bolt wa Siera Lione walishaondoka siku za nyuma. ina maana zimebaki nchi tatu zenye washiriki waliokamilika Tanzania (Nando & Feza), Zambia (Sulu & Cleo) na Nigeria (Melvin & Beverly) nchi zilizobaki Botswana,Namibia na Afrika kusini kuna mshiriki mmoja mmoja tu.

Nani ataibuka na kitita na kuibuka kidedea? Tuzidi kuwapigia kura washiriki wetu Feza na Nando waendelee kubaki mjengoni.

0 Maoni:

Toa Maoni