Kasheshe:Diamond na sakata la Prezzo

Hivi karibuni kumeibuka kumeibuka kutoelewana kati ya mwanamuziki Diamond na Prezzo kisa kikianzia kwenye majigambo waliyotoa kabla ya Tamasha la matumani.Sote tunajua kunapokuwa na mpambano ili kunogesha mambo lazima kuwe na tambo za wahusika ili kuleta ladha zaidi kitu kinachorusiwa maana hata mabondia huwa wanafanya hivyo,wacheza mpira vilevile.

Prezzo
Diamond


Kitendo cha Diamond kujigamba atamgaragara Prezzo kwa perfomance ambao atadodondosha katika tamasha la matumaini yalionekani kumkera mkali kutoka Kenya Prezzo na kupitia akaunti yake ya twitter akafikia hatua ya kumshambulia Diamond na hata kumuita Domo! Mashabikia wa Diamond hawakumuacha wakamshambulia hasa kwa kitendo alichofanya kitu kilichompelekea kutaka kuomba msamaha kwa kumpigia simu Diamond nae hakupokea inawezekana sababu ya hasira pia.
Baada ya beef hilo mtangazaji wa Citizen Kenya Mzazi Willy Tuva alijaribu kuwasuluhisha lakini Diamond akasema hawezi kukubali msamaha wa Prezzo mpaka akaombe kwenye Twitter akimaanisha sehemu aliyotumia kumdhalilisha na Prezzo akagoma na kusema hawezi kufanya huo utoto (wa kuomba msamaha kupitia twitter)! Na hapo chini ni jinsi Prezzo alivyomshambulia Diamond ..


  Na hapa shabiki mmoja aliuliza kama anaenayezungumziwa ni Diamond,jibu hilo hapo..
Kwa hisani ya mtandao wa Kenyan post Diamond anasema hana muda na wa malumbano na Prezzo kitu kitachompotezea muda wa kusaka dough (pesa).

Iliwahi kuripotiwa Diamond ni msanii anayelipwa vizuri sasa Afrika mashariki.Na tukirudi kwenye ukweli kijana anatisha kwa kazi nzuri na mafanikio anayo pia..Hongera kwa hilo Diamond. Swali ni kwamba unafikiri ni majigambo tu aliyotoa Diamond wakati wa Tamasha la matumani ndio yaliyozua yote au ni mafanikio aliyonayo Diamond yamesababisha yote hayo?

0 Maoni:

Toa Maoni