MKASA WA KWANZA: MKE ANAYEFANYA MAPENZI NA ASIO WAJUA USINGIZINI
Mwaka 2004, mwanamke mmoja wa nchini Australia mwenye umri wa makamo, alikuwa akikabiliwa na ugonjwa wa kutembea huku amelala na katika hali ya kushangaza alikuwa akifanya mapenzi na watu asiowajua huku akiwa hajijui kama anafanya hivyo.
Tabia ya mwanamke huyo iliendelea kwa miezi kadhaa bila mwanamke huyo kujua nini huwa anafanya nyakati za usiku akiwa usingizini. Kuzagaa kwa kondomu kwenye eneo la nyumba yao kulimfanya mwanamke huyo na mumewe wakae wajiulize kulikoni.
Kuna siku mumewe alishtuka usingizini na kumkuta mkewe hayupo kitandani alipotoka kumtafuta hadi nje ndipo alipomkuta akifanya mapenzi na mwanaume asiyemjua.Mzozo wa ndoa yao ulitatuliwa na madaktari waliothibitisha kuwa kitendo hicho cha mwanamke huyo kilikuwa ni cha tatizo za kutembea usingizini.
Madaktari wa saikolojia walimpa ushauri nasaha mwanamke huyo na mwanamke huyo alipona tabia yake bila kutumia dawa ya benzodiazepines ambayo hupewa watu wenye tatizo la kutembea huku wamelala.
MKASA WA PILI: MPISHI ANAYEPIKA AKIWA USINGIZINI
Robert Wood, mpishi mwenye umri wa miaka 55 alikuwa akiamka mara nne au tano usiku kwa wiki huku akiwa usingizini hutembea na kuelekea jikoni ambako huanza kupika chapati za maji na chipsi.
Robert amekuwa akiamka na kutembea akiwa usingizini kwa miaka 40 na mkewe Eleanor, amekuwa akihofia sana ajali za jikoni ambazo zinaweza kumpata mumewe.
Robert na mkewe wanaishi Glenrothes, Scotland na hadi hivi sasa hawawezi kulala zaidi ya masaa matatu pamoja bila mumewe kuamka na kuelekea jikoni.
Robert anaamini kuwa matatizo ya tumbo yanayomfanya awe anakula kidogo sana ndiyo yanayomfanya aamke usingizini kila anaposikia njaa. Inasemekana kuwa hadi sasa Robert bado anatafuta matibabu kutoka kwa wataalamu wa masuala ya usingizi mjini Edinburg.
MKASA WA TATU: MWANAUME ANAYEKATA MAJANI AKIWA UCHI.
Mwaka 2005, mtaalamu mmoja wa kompyuta aliyejulikana kama Ian alikutwa na mkewe saa nane za usiku akikata majani kwenye bustani mbele ya nyumba yao kwa kutumia mashine ya kukatia majani akiwa uchi wa mnyama.
Mkewe Rebekah Armstrong alishtushwa usingizini na kelele za mashine hiyo na alipoamka alimkuta mumewe hayupo kitandani na kuamua aende kwenye bustani yao kuangalia nini kinaendelea.Rebekah alimkuta mumewe akikata majani kwa kutumia mashine ya kukatia majani huku akiwa uchi wa mnyama.
Aliogopa kumuasha kwakuwa alishawahi kuambiwa mwanzoni kuwa ni hatari kumshtua mtu anayetembea huku amelala. Alichofanya Rebekkah ni kuichomoa plagi ya mashine hiyo kutoka kwenye swichi na kurudi chumbani kwake kulala.Ian aliendelea kuzunguka na mashine hiyo bila kujua imezimwa na baada ya muda kupita alirudi chumbani na kumalizia usingizi wake.
Asubuhi alipohadithiwa na mkewe kituko alichofanya na ilivyokuwa alibaki mdomo wazi haamini kama ni kweli anaweza kufanya hivyo.
MKASA NAMBA NNE: MWANAMKE ANAYETUMA EMAIL AKIWA USINGIZINI
Mwaka 2005 mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 44 alienda kulala kwenye majira ya saa nne usiku na aliamka baada ya masaa mawili baadae. Aliwasha kompyuta na kusign in kwenye email yake na kuanza kuwatumia watu email tatu.
Maandishi katika email hizo yalikuwa hayaeleweki na yalikuwa mchanganyiko herufi kubwa na ndogo.Katika maandishi ambayo yaliweza kusomeka yalisema "Njoo kesho na utengeneze hili shimo la moto. Chakula cha jioni na vinywaji saa 10.. ". Katika email nyingine aliandika "Nini ...".
Mwanamke huyo alikuwa hajui kama aliamka usiku na kutuma email hizo. Wataalamu wanaita aina ya tatizo hilo la kutembea na kutuma email usingizini "zzz-emailing" na huwapata sana sana watu ambao hutumia muda mwingi kuandika na kutuma meseji au kuchapa barua kama masekretari.
MKASA NAMBA TANO: APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJARIBU KUBAKA
Mwaka 2007, Alan Ball alienda kwenye mkesha wa mwaka mpya na alikunywa sana na hatimaye kupitiwa na usingizi kwenye sofa.
Kuna wakati katika usingizi wake alinyanyuka kwenye sofa na kuanza kutembea kuelekea kwenye vyumba vya juu ya jengo hilo na kupanda kitandani alipokuwa amelala binti yake mwenye umri wa miaka mitano na kuanza kumbusu mdomoni.
Baada ya mwaka mzima wa kutakiwa na mahakama kumtembelea binti yake huyo chini ya uangalizi maalumu, hatimaye mahakama iliamua kumuondelea adhabu hiyo baada ya kuridhika kuwa alifanya kitendo hicho akiwa usingizini na alikuwa hajui atendalo.
Nimeikuta hii mtandao wa Nifahamishe nikaipenda na kuamua ku share na wewe msomaji wa Mamu Africa Blog. Kikawaida kabisa kuna baadhi ya watu wana tabia ya kufanya vitu kama kutembea usingizini!
0 Maoni:
Toa Maoni