Mambo yanaelekea kutoenda vizuri sana kwa mzee wa TAKEU style Mr. Nice alipo namaanisha nchini Kenya pamoja na kupata deal ya kufanya kazi zake za muziki chini ya label mpya inayojulikana kama Candy records.
Weekend iliyoisha ilikuwa mbaya kwa Mr. Nice baada ya kuzomewa na mashabiki huko Kericho Kenya alipokwenda kupiga show.Kwa mujibu wa vyanzo vya habari inaonekana mashabiki hawakuridhishwa na perfomance ya Mr. Nice na kum-boo ashuke jukwaani kitu kilichomfanya aondoke eneo la tukio bila malipo!
Nice na promota wake ambao walikuwa kwenye gari moja walikwama njiani baada ya gari kuishiwa mafuta na kukaa masaa machache kabla ya kupata msaada..mambo si mazuri bora urudi nyumbani Nice bado tunakupenda.

0 Maoni:
Toa Maoni