1: Ana asili ya mmanyema, mfipa na Mrusi.Baba yake Nelly ni mtanzania halisi kabisa akiwa amechanganyika Mmanyema pamoja na mfipa ila mama yake ni Mrusi kabisa akiwa na uraia wa Tanzania.
2:Ana vipaji vingi alivyobarikiwa..ni bell dancer anajua kucheza, anajua kuimba pia ni mwanamitindo.
3:Alianza kushiriki mashindano ya urembo akiwa na umri wa miaka 16 tu bila waandaji kujua hilo na anasema alifika kwenye nafasi kumi bora ila umri ndio ulimuangusha kunyakuwa taji kwa kuwa vigezo alikuwa navyo.Anakiri alipata experience ya kutosha kutokea hapo.
4:Ameshawahi kurekodi wimbo wake mwaka 2011 ambao aliuweka You tube kwa ajili ya watu wa nchi tofauti kuuona kutoa maoni na kupata msukumo zaidi wa kumpigia kura za kumwezesha kushinda taji la miss universe. Wimbo huo SAY IT TO MY FACE aliufanya Bongo record chini ya producer P Funk Majani ambapo asilimia kubwa katumia lugha kingereza kuimba.
Nelly kazungumzia pia kilichompandisha stejini katika Tamasha la matumaini na rapa kutoka Kenya Prezzo na kusababisha mshtuko kwa baadhi ya watu. Amefahamiana na Prezzo kupitia msaniiAY ambaye anasema walikutana kiwanja kipindi Prezzo yuko TZ wakasalimiana tu na kupiga picha na baadae Prezzo akavutiwa kufanya nae kazi baada ya kupata habari zake baada ya kukutana. Na kzi ya kwanza ikaonekana Tamasha la matumaini.
Anasema ana mpango wa kuendeleza kipaji cha kuimba kwa kufanya ngoma nyingine kali siku za usoni.



-5.jpg)


0 Maoni:
Toa Maoni