Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 za Tanzania.Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.Nzoa alisema Jeshi la Polisi Nchi linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
![]() |
| Melisa Edward |
Sasa inasemekana Agness Jerald ni yule binti maarufu video qeen hapa bongo akijulikana zaidi kama Agnes masogange. Mara kadhaa amekuwa akipost picha Instagram zikimuonyesha anakula bata Afrika kusini! Swali likawa binti huyo ana ishu gani inayomuwezesha kupata pesa za kula bata hivyo na kupiga tripu za kwenda na kurudi kila mara!
![]() |
| Kazi kweli kweli |
Wengine wakiona hivi nao wanaanza michakato ya kuiga bila kujua nyuma ya pazia kunani! Hii ni akaunti ya Agnes intagram ilivyoandikwa..
Siku si nyingi tulipata taarifa ya binti wa kitanzania Fatma kukamatwa nchini Misri na madawa ya kulevya yaliyokuwa kwenye begi lake la nguo.Alisema hajui dawa hizo zimefikaje kwenye begi lake wakati akihojiwa ila vitu vilikuwa katika himaya yake!
Majanga haya imekuwa kawaida sasa kuyasikia kila mara wahusika wakuu wakiwa vijana! Hivi ni kutafuta urahisi wa maisha au ni uvivu wa vijana kufanya kazi au ni tamaa? Majangaa tusaidiane katika hili tunaelekea kubaya.
![]() |
| Fatma akiwa chini ya ulinzi |

.jpg)


0 Maoni:
Toa Maoni