Akiongea na Times fm Fred Mariki maarufu kama Mkoloni kutokea msibani amesema mama Jay baada ya kugongwa na gari alimpigia simu mwanae kumwambia amepata ajali jambo lilimpa matumaini msanii huyo kwa kufikiri huenda hali ya mama yake haikuwa mbaya sana. Walipompeleka hospitali ya Tumbi Kibaha ndio ikathibitishwa ameshafariki dunia.
Msiba uko Mbezi mwisho nyumbani kwa Profesa J na mipango ya mazishi inaendelea.Mamu Africa blog inatoa pole kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.

0 Maoni:
Toa Maoni