Waziri mkuu mpya wa Misri,Hazem al-Beblawi anaanza kibarua cha kuteua baraza la mawaziri ,ikiwa ni wiki moja baada ya kuondolewa madarakani kwa rais Mohammed Morsi.
El Beblawi amesema atatoa viti kadhaa vya uwaziri kwa chama cha Muslim Brotherhood kinachoongozwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chama hicho amesema hawatashiriki katika muungano wa serikali yoyote hadi pale kiongozi wao Mohammed Morsi atakaporejeshwa madarakani.
Ratiba iliyotolewa ya maandalizi ya uchaguzi mpya, ilitangazwa na rais wa muda, Adly Mansour Jumatatu ikiwa ni saa kadhaa baada ya watu 51 kuuawa wengi wao wakiwa wa chama cha Muslim Brotherhood,waliouawa wakiwa nje ya kambi ya jeshi wanakoamini kuwa Morsi anazuiliwa.

0 Maoni:
Toa Maoni