Meneja biashara wa mshindi huyo wa 2012 BET Best International Act (Africa) Sammy Forson amesema mwanamuziki huyo yupo salama.
![]() |
| Sarkodie na mama yake |
Jana jioni mitandao ya kijamii ilitawaliwa na uvumi kuwa msanii huyo amefariki na wengine wakisema amefariki kwenye ajali ya gari iliyotokea Kintampo road,kwenye mkoa wa Brong Ahafo.
Sarkodie na meneja wake baada ya taarifa hizo,haraka kwa kupitia Twitter wakazungumzia uvumi huo wakiuita usio na maana.
Uvumi huo umekuja siku chache baada ya kuachia ngoma yake ya Elijah iliyomo kwenye albam yake mpya ya Sarkology.

0 Maoni:
Toa Maoni