Baada ya mshiriki wa Big Brother The Chase Beverly Osu,kudai kuwa amewahi kupigwa na mpenzi wake wa zamani rapper ambaye hakumtaja jina,hatimaye mpenzi wake wa zamani ambaye ni rapper 2shortz amejibu madai hayo ya mwanadada huyo.
Beverly akiwa ndani ya jumba la Big Brother alisema mpenzi wake huyo amewahi kumpiga kipigo kikali mpaka akakimbilia bafuni ambako nako mpenzi huyo alimfuata na kuvunja mlango kisha kumuendelezea kipigo.
Japo Beverly hakutaja jina lakini inaeleweka kuwa mwanadada huyo amewahi kutoka kimapenzi na rapper 2shotz,haieleweki kama ndiye alikuwa anamlenga au alikuwa anamzungumzia rapper mwingine lakini wengi wanaamini aliyekuwa anamzungumza ni 2shotz.
Rapper huyo amesema madai hayo ni uzushi ambao unasambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye blogs na baada ya kupata ujumbe kutoka kwa mashabiki wake,marafiki na familia ameamua kufunguka na kuweka ukweli wake kuwa hakuwahi kumpiga Beverly wala mwanamke yeyote katika maisha yake na wala hatarajii kufanya hivyo na kuwataka mashabiki wake,marafiki na familia yake kupuuza habari hizo za uongo.
Hiki ndio alichoandika 2shotz kuhusu madai hayo dhidi yake ya kumpiga Beverly.


0 Maoni:
Toa Maoni