KIOJA: Apandisha maruhani kisa biashara ya pombe za kienyeji


Mama mmoja ambaye ni mfanyabiashara wa pombe za kienyeji hivi karibuni aliwaacha vinywa wakazi wakati wa Tungi Kigamboni baada ya kudaiwa kupandisha mashetani na kisha kwenda kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara mwenzake wa pombe za kienyeji akidai kuwa ni mshirikina.
Hili ndilo eneo ambalo shimo lilichimbwa kwa ajili ya kutoa mtoto aliyedaiwa kufukiwa
Ingawa katika maelezo yake na mashuhuda walidai mama huyo hakumtaja mtu jina lakini ni dhahiri kwamba mama huyo alimdhamiria jirani yake huyo kutokana na kumuhusisha mtoto wake ambaye wakati tukio linatokea alikuwa amelala.
Mama aliyepandisha mashetani akiwa ameshika gogo alilodai ndio mtoto aliyefukiwa
“Kusema ukweli huyu mama hukumtaja mtu jina lakini kitendo chake cha kwenda nyuma ya chumba cha jamaa sanjari na kumwamsha mtoto wake na kumtaka kwenda nae kuangalia kilichofukiwa na baba yake ni kama ndio alikuwa anathibitisha kwamba huyu jamaa kuwa ni mchawi!” alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo.

Sakati hilo ambalo kwa sasa lipo katika ofisi za serikali za mtaa Muungano Tungi Kigamboni, limesababisha jamaa huyo kutimuliwa na baba mpangaji wake sambamba kuwa na hofu na maisha yake kutokana na tukio hilo.

“Kwasasa nimeshahamishwa pale nilipokuwa nakaa kutokana na tukio hilo lakini pia kwa sasa maisha yangu yapo rehani na watu wanajua kweli mimi ni mshirikina kitu ambacho si kweli sasa naomba serikali watatue tatizo hili haraka maana watu wananing’ong’a” alisema mtuhumiwa huyo wa uchawi. 
Jamaa aliyedaiwa ni mchawi akiwa na mkewe katika mahojiano na Edson Mkisi Jr
Mama mpandisha majini alidai hakudhamiria kufanya tukio hilo na yeye si mganga bali ni kweli alipandisha majini na ndio waliomtuma kwenda kufukia kitoto hicho ambacho katika macho ya kawaida alidai huwezi kumuona ila ataonekana kama gogo.

Aidha, Mjumbe wa serikali za Mitaa Muungano Athuman Hamisi alisema tukio hilo limesharipotiwa kwenye ofisi yao lakini kutokana na tukio hilo kuhusisha imani za kishirikina hakuna wanachoweza kusema kutokana na ukweli mkwamba serikali siku zote haiamini ushirikina. 
Mjumbe wa serikali za mitaa ambaye ni baba mwenye nyumba
Kwa tukio kamili sikiliza Kipindi cha Hatua Tatu kesho kupitia Times fm 100.5
Ahsante kwa Edson Mkisi Jr ''Digital" kwa stori hii.

0 Maoni:

Toa Maoni