![]() |
| Miye,Kelvin na Elizabeth |
Akizungumzia kikubwa alichofanyia sehemu iliyobaki ya fedha hizo Kelvin amesema yeye na mke wake Elizabeth wamefungua mgahawa mkubwa nchini Nigeria ambao unauza vyakula mbalimbali vya KiNigeria na kiTanzania.
Naye Elizabeth amesema mbali ya vitega uchumi ambavyo wamefungua nchini Nigeria kwasasa wanafikiria jinsi ya kuweka miradi mbalimbali Tanzania ikiwemo kuanzisha shindano la kusaka vipaji ambalo kwa Nigeria limefanya vizuri.
Aidha amesema akiwa nchini Nigeria anaendelea pia na shughuli mbalimbali ikiwemo kucheza filamu na nyota mbalimbali wa nchini humo.
Wakati huo huo Kelvin akafunguka kuwa mke wake Elizabeth ndiye mwanamke anayejua zaidi kupika kuliko wanawake wote aliowahi kutoka nao kimapenzi.




0 Maoni:
Toa Maoni