PICHA : Kiota cha Samaki Samaki kikiteketea na moto mchana huu


Kiota cha Samaki Samaki kilichopo Mbezi eneo la Makonde kimeteketea kwa moto mchana huu uliotokana na tinga tinga za bomoa bomoa kusababisha shoti ya umeme.

Tinga tinga hizo za bomoa bomoa zilifika eneo la tukio kwaajili ya kubomoa sehemu ya hifadhi ya barabara zoezi ambalo limekuwa linaendelea la upanuzi wa barabara ya Bagamoyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema dereva wa tinga tinga alielezwa kuwa kuna cheche zinatoka kwenye kiota hicho cha Samaki Samaki ambacho makuti yaliyoezekwa yaligusa nyaya za umeme nakusababisha shoti hiyo ambayo kama si ubishi wa dereva huyo moto usingetokea.

Dereva wa tinga tinga akarudi kwa mara ya pili na ndipo makuti yaliposhika moto ambao ukateketeza kiota hicho na ukashika kwenye jengo lingine la pembeni yake ambalo lina ofisi za kampuni ya ujenzi ya Xenco.
 
 
Magari ya kikosi cha Zimamoto yalipofika eneo la tukio kama kawaida gari lao likawa halina maji na ikalazimika lori kubwa la kubebea maji kuitwa haraka na kujaza maji kwenye gari hilo la Zimamoto lenye namba za usajili STK 2691.
 
Zoezi la kuzima moto likaendelea.
 

Kabla ya Kikosi cha Zimamoto kufika eneo hilo la tukio moto huo ukawa unazimwa kwa kutumia ndoo za maji.
 

Kama ilivyo kwenye matukio mengi yanayotokea wananchi nao wakajitokeza eneo la tukio wakitazama moto unavyoteketeza kiota hicho cha Samaki Samaki.

 
Kampuni ya ujenzi ya Xenco wakaamua kuokoa mali zao kabla hazijateketea japo kuna baadhi tayari ziliteketea kwa moto huo.

0 Maoni:

Toa Maoni