Msanii mkongwe aliyeamua kupumzika kwenye muziki baada ya kuutumikia kwa miaka 53 Maalim Gurumo amezawadiwa gari aina ya Funcargo na msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul DIAMOND.
Gurumo aliyekuwa akitangaza kustaafu muziki huku akimwaga chozi,alisema anastaafu muziki huku akiwa hana hata Baiskeli katika miaka yote hiyo aliyoutumikia muziki ambao bado anaupenda.
Diamond ameguswa na maneno ya Maalim Gurumo na kumzawadia gari hiyo jana kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Number One uliofanyika kwenye hoteli ya Serena.
Msanii huyo amefanya jambo kubwa ambalo wengi wanaona itamuongezea baraka na kuendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki.
Cheki baadhi ya picha ya waliohudhuria.
 |
| Dully & Shadee |
 |
| Mama Diamond alikuwepo |
 |
| Penny & Diamond |
 |
| Sauda na Chege |
 |
| Shaa na madam Ritha |
 |
| Irene Uwoya |
Kutoka Mamuafrica blog tunampa hongera sana Diamond kwa moyo wa kutoa na upendo aliouonesha kwa msanii huyo mkongwe.
0 Maoni:
Toa Maoni