Rais Uhuru Kenyatta kuwa mgeni katika uzinduzi wa album ya Miss Karun

Aliyekuwa member na first lady wa kundi kutoka Kenya linalofanya vizuri na kujichukulia umaarufu mkubwa Africa Camp Mulla, Miss Karun anatarajia kuzindua album yake ya kwanza akiwa kama solo artist baada ya kundi lao kuvunjika mapema mwaka huu.
Camp Mulla
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo na kumfanya Miss Karun kwa kipindi kifupi alichokaa kwenye fani kuweka historia ya kuwa Mkenya wa kwanza kuwa na Rais katika uzinduzi wa album yake na pia kuwa nominated katika tuzo za BET.

Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akijichanganya katika mambo mbalimbali ya kijamii  na hata kiburudani na habari hiyo ya Rais kuhudhuria uzinduzi imetolewa na mwandishi wa habari za serikali huko Kenya Dennis Itumbi kupitia twitter.

0 Maoni:

Toa Maoni