Watanzania mnaombwa kutoa sapoti katika mapokezi ya Feza jioni leo

Aliyekuwa mshiriki wa BBA The chase kutoka Tanzania Feza Kessy anatarajiwa kuwasili leo katika uwanja wa kimataifa wa Mwl J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.Watanzania mnahimizwa kujitokeza kwa wingi kumpokea.Feza Kessy anategemewa kuingia na ndege ya shirika la South African Airways majira ya saa 12:30 jioni.

Tuonyeshe uzalendo na upendo jamani kwa kumpokea mwenzetu maana katuwakilisha vyema mpaka pale alipofikia maana wenzetu washiriki wao wanapokelewa kwa shangwe mpaka mtu anajisikia fahari kuiwakilisha nchi yake si mnakumbuka mapokezi aliyopewa Pokello? Kama hukumbuki cheki baadhi ya picha hapo chini.
Umati uliojitokeza kumpokea  Pokello  uwanja wa ndege wa kimataifa Harare

0 Maoni:

Toa Maoni