Msanii anayekuja kwa kasi kwenye game kwa sasa Snura Mushi amesema silaha yake kubwa ni viuno huku akikataa kufananishwa na mwanadada Shilole aliyeanza kutumbukia kwenye muziki na yeye akafuatia.
 |
| Snura akiwa amepiga pozi |
Snura amesema ameingia katika muziki si kwa kubahatisha ila kwa kupania kufanya kweli kama alivyothibitisha kwenye wimbo wake wa Majanga uliomtambulisha katika tasnia ya muziki.
Amesema anatambua mashabiki wa muziki wanataka nini na ndio maana ameamua kuendelea kujiimarisha zaidi katika style yake ambayo inatumia zaidi kiuno na akasema style hiyo japo inafanana na ile anayotumia Shilole akasema yeye ni mkali zaidi ya wasanii wengine akiwemo Shilole na linapokuja suala la kwenye stage anatisha zaidi.
Alipoulizwa kama ana bifu na Shilole akasema hajawahi kuwa na bifu na mwanadada huyo yeye ana bifu na hela huku akisema yuko tayari muda wowote kushirikiana na Shilole.
 |
| Shilole akifanya mambo yake |
0 Maoni:
Toa Maoni