Wema Sepetu anaplan ya kufanya muziki?

Kila anachofanya aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania Wema Isaac Sepetu aliyegeukiwa kwenye filamu kimeendelea ku make headlines katika media na hata mitandao ya kijamii.

Jana kupitia mtandao wa  Instagram jana mrembo Wema Sepetu alipost picha yake kisha chini akaandika mashairi matamu ya kimapenzi.. "Mwambie wake ni mimi, na kwangu moyoni atabaki ni yeye, tena mwambie bado silali kutwa nawaza penzi langu...ila siku atagundua kuwa mi ndo mwenyewe..(wanna start singing now)" kitu kilichozua gumzo watu wakijiuliza ni kweli mwanadada huyu anataka kuingia kwenye muziki!

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii wa filamu kama Shilole,Snura, Flora Mvungi,Mzee Magali na wengineo kuingia katika muziki,kwa hiyo si ajabu kusikia Wema Sepetu akiachia ngoma yake.


0 Maoni:

Toa Maoni