Binti afariki kwa kufanya tendo la ndoa na mumewe

Binti wa miaka nane aliyeolewa Yemen amefariki baada ya kuumia kwa ndani katika usiku wa ndoa yake baada ya damu kuvuja ukeni wakati wa tendo la ndoa na mume wake mwenye miaka 40.

Binti huyo ametajwa kwa jina moja la Rawan,amefariki huko Hardh jimbo la Hajjah Kaskazini magharibi mwa Yemen.

Wanaharakati wa Yemen wanataka kumalizwa kwa vitendo vya mabinti kuolewa katika umri mdogo na wamewataka Polisi kumkamata mume wa binti huyo na familia yake.

Wamesema ni lazima mume huyo na familia ya binti waburuzwe mahakamani ambako sheria itachukua mkondo wake na itasaidia kukomeshwa kwa vitendo vya ndoa za lazima kwa mabinti wadogo.


0 Maoni:

Toa Maoni