Dibibi amesema tokea ameingia kwenye ndoa na nyota huyo wa filamu amekuwa anafurahia maisha na mapenzi anayopata kutoka kwake akitumikia ndoa yake kama mke anayejua majukumu na wajibu wake.
Dibibi amefunguka zaidi akisema amekuwa karibu na mke wake na wakishirikiana katika mambo mengi kiasi hata password kila mmoja anafahamu ya mwenzake,iwe ya bank au hata kwenye mitandao ya kijamii ya facebook na twitter,na hata simu zao kila mmoja yuko huru na simu ya mwenzake jambo ambalo linaongeza uaminifu kwao.
Amesema watu hawapaswi kumfikiria tofauti mke wake kwakuwa amebadilika na mwenye kujua wajibu wa mke,huku akisema mambo ya nyuma ya mke wake hataki kuyaafuatilia kwakuwa hata yeye akifuatiliwa ya nyuma anaweza kuwa sio msafi.
Akiwafunga watu midomo Dibibi amesema maisha yake na Jack yanakwenda safi na wanafurahia ndoa yao,akiwataka watu kuacha maneno ya kufuatilia ndoa yao na kusema vibaya,kikubwa ni wao wanapendana kwa dhati ya mioyo yao.


0 Maoni:
Toa Maoni